1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Manchester City yatinga fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya

18 Mei 2023

Mashabiki wa kandanda hapo jana walistareheshwa kwa mechi za nusu fainali barani Afrika na hapa barani Ulaya.

https://p.dw.com/p/4RXS8
Champions League | Real Madrid - Manchester City
Picha: Jason Cairnduff/Action Images/Reuters

Mashabiki wa kandanda hapo jana walistareheshwa kwa mechi za nusu fainali barani Afrika na hapa barani Ulaya.

Katika nusu fainali ya pili ya ligi ya mabingwa wa Ulaya, timu ya Manchester City ya Uingereza iliichabanga Real Madrid ya Uhispania mabao 4-0 na kutinga katika fainali ambapo itapambana na Inter Milan ya Italia, iliyoibagwa AC Milan, bao 1-0 hapo siku ya Jummane katika nusu fainali ya kwanza.

Na barani Afrika wawakilishi wa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika Yanga Sports Club ya Tanzania imefanikiwa kutinga kwenye fainali ya michuano hiyo baada ya kuipangua klabu ya Marumo Galants ya Afrika Kusini kwa jumla ya magoli 4-1 katika michezo miwili ya nyumbani na ugenini.

Yanga watakutana katika mchezo wa fainali na USM Alger, kutoka Algeria ambao nao wametinga fainali baada ya kuiondosha ASEC Mimosas ya Ivory Coast kwa jumla ya magoli 2-0.

Mchezo wa kwanza wa fainali utachezwa Mei 28 na ule wa marudio utachezwa Juni 03 mwaka huu. Yanga wataanzia nyumbani na kumalizia ugenini.