1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUingereza

Man United yatinga kwa raundi ya 16 bora ligi ya Ulaya

24 Februari 2023

Manchester United imepangwa na Real Betis katika hatua ya 16 bora siku ya Ijumaa katika ligi ya Ulaya, hii ni baada ya kuibandua Barcelona kwa kipigo cha mabao 2-1.

https://p.dw.com/p/4Nwzj
Fußball I Manchester United v Arsenal - Premier League - Old Trafford
Picha: Martin Rickett/empics/picture alliance

Manchester United mshindi wa mwaka 2017, watawaalika Real Betis katika uga wa nyumbani Old Trafford mnamo Machi 9.

Shakhtar Donetsk timu ya pekee iliyobakia katika michuano ya ligi ya Ulaya imefuzu kwa raundi ya 16 bora na kupangwa na Feyenoord. Shakhtar itakuwa mwenyeji wa mkondo wa kwanza dhidi ya Feyenord katika nchini jirani Poland kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Vinara wa Ligi Kuu ya Premier Arsenal watamenyana na Sporting Lisbon, na mkondo wa kwanza utachezwa Ureno.

Britain Soccer Premier League Arsenal vs Chelsea
Bukayo Saka- Mchezaji wa ArsenalPicha: Andre Boyers/AP/picture alliance

Juventus imeorodheshwa kuchuana na Freiburg na bingwa mara sita Sevilla watakuwa nyumbani kwanza dhidi ya Fenerbahce. Union Berlin itakutana tena na Union Saint-Gilloise baada ya kukutana mara mbili katika hatua ya makundi.

Roma, chini ya mkufunzi Jose Mourinho, itacheza na Real Sociedad, huku Bayer Leverkusen ikitarajia kuvaana na Ferencvaros.

Ferencvaros watakuwa wenyeji wa mkondo wa pili kwenye uwanja wa Puskas Arena Budapest, uwanja ambao pia utaandaa fainali ya Ligi ya Uropa Mei 31.

Katika mechi nyingine, West Ham itasafiri hadi Cyprus kwa mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya AEK Larnaca, Sheriff itakuwa mwenyeji wa Nice huko Moldova, na Lazio itakuwa nyumbani kuanza dhidi ya AZ Alkmaar.