1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamlaka ya kijeshi Mali yakataa ripoti ya Umoja wa Mataifa

14 Mei 2023

Serikali ya mpito ya kijeshi ya Mali imeikataa ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu madai ya kunyongwa kwa takribani watu 500 na wanajeshi wa Mali na wapiganaji wa kigeni wasiojulikana wakati wa operesheni mwaka jana.

https://p.dw.com/p/4RL0T
New York | Abdoulaye Maiga, Premierminister von Mali | UN-Generalversammlung
Picha: Mary Altaffer/AP/picture alliance

Mamlaka ya kijeshi ilikuwa ikijibu ripoti hiyo iliyolewa baada ya uchunguzi wa miezi kadhaa kuhusu kile ambacho mashirika ya kutetea haki za binaadamu yameeleza kuwa ni ukatili mbaya zaidi katika mzozo wa miaka 10 kati ya wenye itikadai kali na jeshi.Katika taarifa yake, msemaji wa serikali ya Mali, Abdoulaye Maiga, amesema serikali imeilalamikia sana ripoti hiyo kwa kusema inaegemea upande mmoja kwa kujikita katika uongo na kwamba haikidhi viwango vya kimataifa.Katika tukio la Machi 27 mwaka jana, ripoti hiyo inasema wanajeshi wa Mali na mamluki wa kigeni walitua kwa helikopta katika kijiji cha Moura na kuwafyatulia risasi wakaazi waliokuwa wakikimbia. Na katika siku zilizofuata matendo kama hayo yaliendelea kufanyika na miili ya watu kutupwa katika mitaro.