1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiTunisia

Mamia ya wahamiaji wa Kiafrika waikimbia Tunisia

4 Machi 2023

Raia 300 wa Ivory Coast na Mali wanatarajiwa kuhamishwa kutoka Tunisia leo, kufuatia wimbi la mashambulizi dhidi ya wahamiaji wanaotokea mataifa ya kusini mwa Jangwa la Sahara baada ya kauli yenye utata ya Rais Saied.

https://p.dw.com/p/4OFes
Tunesien Tunis | Demo gegen Rassismus
Picha: Fauque Nicolas/Images de Tunisie/abaca/picture alliance

Mashirika ya kutetea haki za binaadamu yameripoti kuongezeka kwa vitendo vya kushambuliwa kwa raia hao wa kigeni. Jean Bedel Gnabli, naibu mkuu wa chama cha wahamiaji amesema watu wanaishi kwa hofu.

Vitendo hivyo, ikiwa ni pamoja na kuchomwa visu vimeongezeka baada ya Rais Saied kuwataka maafisa kukabiliana na uhamiaji haramu akidai kuna njama ya kuubadili muundo wa jamii ya watu wa Tunisia.

Soma zaidi: Wanaharakati wamkosoa rais wa Tunisia

Umoja wa Afrika umetaja kushtushwa na kuwa na wasiwasi juu ya matamshi hayo ya Rais Saied.