1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamia wapoteza kazi baada ya jeshi kufungia vituo vya habari

29 Mei 2024

Mamia ya watu wamepoteza nafasi zao za ajira baada ya utawala wa kijeshi nchini Guinea kuvifungia vituo vinne vya redio na viwili vya televisheni.

https://p.dw.com/p/4gQqv
Conakry, Guinea |
Mamia wapoteza kazi baada ya jeshi kufungia vituo vya habariPicha: John Wessels/AFP

Hayo yameelezwa na muungano wa vyombo vya habari ambao unajiandaa kuitisha mgomo wa nchi nzima.

Muungano huo siku ya Jumatatu ulitishia kuanzisha mgomo wa nchi nzima usiokuwa na kikomo baada ya mamlaka nchini Guinea kufuta leseni za uendeshaji wa shughuli za vituo sita vya habari wakati nchi hiyo ikiwa inakabiliwa na wasiwasi wa kijamii na mazingira mabaya ya kisiasa.

Muungano huo wa SPPG  umevitaka vyama vyote vya wafanyakazi kupitia barua iliyoonekana leo na AFP, kuunga mkono mgomo huo.

Mamlaka zimesema kufungiwa vituo hivyo vya habari  kumetokana na vyombo hivyo kushindwa kutekeleza maagizo kuhusu maudhui wanayorusha hewani.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW