1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUturuki

Mamia waandamana Uturuki kupinga mauaji ya wanawake

13 Oktoba 2024

Mamia ya wanawake wameandamana katika miji mbalimbali nchini Uturuki ikiwa ni pamoja na mji mkuu Ankara na Izmir kupinga mauaji ya wiki iliyopita ya wanawake wawili mjini Istanbul.

https://p.dw.com/p/4ljLU
Maandamano Uturuki katika siku ya kimataifa ya wanawake
Maandamano Uturuki katika siku ya kimataifa ya wanawake Picha: Khalil Hamra/AP Photo/picture alliance

Kwa karibu wiki moja sasa, kote nchini Uturuki kumekuwa kukishuhudiwa kila siku maandamano kama hayo haswa kwenye vyuo vikuu. Waandamanaji waliimba nyimbo za kumshutumu Rais Recep Tayyip Erdogan na chama chake cha AKP wakisema ni serikali inayowaacha wasichana wadogo kuuawa.

Erdogan alisema pombe na mitandao ya kijamii ndio chanzo cha mauaji hayo huku akiahidi kuimarisha mfumo wa haki na kukabiliana na uhalifu. Hata hivyo  Uturuki imeshindwa kukabiliana na mauaji ya wanawake.  Kundi moja la wafuatiliaji linasema kumekuwa na wanawake 299 waliouawa mwaka huu katika nchi hiyo yenye watu milioni 85, huku mauaji mengine 160 yakishukiwa na kutajwa rasmi kuwa ni vitendo vya kujiua au ajali.