1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamia waandaman kumkumbuka miaka 3 ya mlipuko wa Beirut

5 Agosti 2023

Mamia ya watu jana waliandamana nchini Lebanon katika kumbukumbu ya miaka mitatu tangu kulipotokea mlipuko mkubwa mjini Beirut. Tangu wakati huo hakuna hata mtu mmoja ambaye amewajibishwa kuhusu mkasa huo.

https://p.dw.com/p/4Uo0N
Maandamano ya kumbukumbu ya miaka mitatu tangu ulipotokea mlipuko Beirut
Maandamano ya kumbukumbu ya miaka mitatu tangu ulipotokea mlipuko BeirutPicha: Hassan Ammar/AP/picture alliance

Mnamo Agosti 4 mwaka 2020, bandari ya Beirut ilitikiswa na mlipuko mkubwa ulioharibu maeneo ya mji huo mkuu na kuwaua zaidi ya watu 220 na kujeruhi wengine takribani 6,500.

Soma zaidi: Lebanon: Uchunguzi kubaini iwapo mkono wa nje ulihusika

Mamlaka zinasema kwamba janga hilo lilisababishwa na moto katika ghala ambako shehena ya mbolea ya amoniam nitrate ilikuwa imehifadhiwa kwa miaka mingi. Waandamanaji, wengi wakiwa wamevalia nguo nyeusi na kubeba picha za wahanga, walikusanyika kuelekea eneo la bandari wakisema kuwa hawatosahau.

Mlipuko huo ulitokea wakati Lebanon ikiwa katika hali mbaya ya kiuchumi.