1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Malta. Watu 27 wafamaji katika bahari ya Mediterranean wakati wakijaribu kuingia Ulaya kutoka Afrika.

25 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF0L

Wahamiaji 27 wanahofiwa kuwa wamekufa baada ya chombo walichokuwa wakisafiria kuzama katika bahari ya Mediterranean karibu na kisiwa cha Malta.

Hakuna kitu kilichopatikana tangu pale watu hao waliokuwa wakisafiri katika chombo hicho kupiga simu ya mkononi kutoa ishara ya hali waliyokuwa nayo kwa walinzi wa eneo la pwani ya Itali wakisema kuwa chombo chao kinazama.

Walinzi hao wa Itali walituma ujumbe wa haraka kwa walinzi wa Malta ambao walianza msako.

Jeshi la majini la Malta limesema kuwa chombo hicho kilitokea nchini Libya.

Mara kwa mara wakati huu wa majira ya joto mamia ya wahamiaji watarajiwa wanajaribu kuingia katika mataifa ya Ulaya kutoka Afrika.