1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Malori kadhaa yamekwama katika mpaka wa Kenya na Tanzania

Veronica Natalis
12 Septemba 2022

Zaidi wa Malori 150 ya mahindi yamekwama katika mpaka wa Namanga uliopo Arusha, unaoziunganisha nchi za Kenya na Tanzania, kwa kile kinachoelezwa kwamba baadhi ya Malori hayo hayana vibali vya kubeba mizigo.

https://p.dw.com/p/4Gj1v
Lori kadhaa zimekwama katika Kituo cha Mpaka cha Namanga
Lori kadhaa zimekwama katika Kituo cha Mpaka cha NamangaPicha: Veronica Natalis/DW

Ni madereva wa magari ya mizigo kutoka nchi za Tanzania na Kenya wakifanya kikao hapa katika mpaka wa Namanga uliopo wilayani Longido mkoani Arusha kaskazini mwa Tanzania ili kujadili vikwazo wanavyokumbana navyo wakati wa kuvuka mipaka hasa mpaka wa Namanga. Madereva hao wanasema serikali za Tanzania na Kenya zinaweza kuweka utaratibu mzuri wa ukaguzi wa magari hayo makubwa ya kubeba mizigo usiokuwa na athari kwa pande zote mbili ili kuondoa vikwazo vya safari mipakani wanavyokabiliana navyo madereva. Mamlaka katika mpaka huo wa Namanga kwa upande wa Tanzania zinasema zinasimamia utaratibu wa ukaguzi wa magari kulingana na maelekezo ya wizara ya kilimo nchini humo. Audax Asheli ni Afisa mfawidhi wa Forodha katika mpaka wa Namanga upande wa Tanzania.

Waziri wa kilimo nchini Tanzania Hussein Bashe aliwahi kuwaambia waandishi wa habari Kamba utaratibu huo wa ukaguzi wa magari makubwa yanayobeba mizigo uliowekwa mipakani pamoja na mambo mengine unalengo la kulinda ubora wa soko la mazao la Tanzania.

Hadi sasa malori yapatayo 150 yaliyobeba mahindi bado yamekwama katika mpaka wa Namanga kufuatia mgogoro huo.