1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mali :Wanamgambo wa GSIM wakubali mazungumzo na serikali

Saleh Mwanamilongo
10 Machi 2020

Kundi kuu la wanamgambo wenye mafungamano na Al Qaeda nchini Mali la GSIM limetangaza kwamba liko tayari kufanya mazungumzo na serikali ya Mali lakini kwa masharti.

https://p.dw.com/p/3ZAfA
Nordmali | Besuch des Premierministers von Mali Boubou Cisse in Kidal
Picha: Pressedienst des Premierministers von Mali

Kundi kuu la wanamgambo wenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda nchini Mali la GSIM limetangaza kwamba liko tayari kufanya mazungumzo na serikali ya Mali lakini kwa masharti. Miongoni mwa masharti hayo ni kuondolewa kwa vikosi vya Ufanrasa na Umoja wa Mataifa vilivyoko maeneno ya kati na ya kaskazini mwa nchi hiyo. Hata hivyo serikali ya mjini Bamako bado kutoa msimamo wake kufutaia pendezo hilo. 

Taarifa hiyo inafuatia pendekezo la rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita ya kutaka kuweko na mazungumzo na kundi hilo la wanamgambo wa kiislamu ili kumalizisha machafuko yalioanza toka mwaka 2012 nchini mwake. ''Tuko Tayari kuanzisha mazungumzo na serikali ya Mali ambayo rais wake alielezea niya ya kuzungumza na kundi letu la GSIM ili kumalizisha machafuko ambayo yanasabishwa pia na uvamizi wa wafaransa'' inaelelezea taarifa iliyotolewa na kundi hilo kupitia mtandao wake wa Al-Zallaqa na kuthibitishwa na kituo cha marekani cha kinachochunguza mitandao ya kigaidi SITE.

''Hatuna masharti mengine kabla ya kushiriki kwenye mazungumzo hayo kuliko yale ambayo kundi la GSIM linayaelezea kuwa ni matakwa ya raia wa mali,ambayo ni kukomeshwa kwa uvamizi wa kibaguzi na wenye kiburi wa wanajeshi wa Ufaransa.,inaelezea taarifa ya kundi hilo la kigaidi. Likiendelea kusema kwamba ''haliwezi kuzungumza ikiwa uvamizi unaendelea na kabla ya vikosi vyote vya ufaransa na washirika wake kuondoka''.

Raia wataka wanajeshi wa Ufaransa kuondoka

Symbolbild- Nigera - Militärübung
Picha: picture-alliance/dpa/P. de Poulpiquet

Msimamo huo wa kundi la GSIM unakuja baada ya maandamano kadhaa ya raia wa Mali kuwataka wanajeshi wa Ufaransa kuondoka nchini humo. Ufaransa ilipeleka wanajeshi wake 5,100 wa kikosi maalumu cha Barkhane kwa ajili ya kupambana na makundi ya kigaidi huko mali na kwenye jimbo la Sahel. Kikosi cha umoja wa mataifa nchini humo kina wanajeshi 12,000.

Maeneo ya katikati na Kaskazini mwa Mali yamekuwa yakipata mashambulizi na vurugu baada ya kupinduliwa kwa serikali mnamo mwaka 2012. Tangu  wakati huo, makundi ya waasi na badaye kundi la kigaidi la Al Qaeda pamoja na wanamgambo wanaoshirikiana nalo wamekuwa wakishambulia eneo hilo.Eneo la Sahel, ambalo ni jangwa kubwa katika eneo la Afrika Magharibi, linatajwa kuwa makazi ya makundi kadhaa yaliyo na ufungamano na makundi ya kigaidi ya Al-Qaeda na Islamic State.

Pia kuna wanamgambo wa kikabila wanaopigana wenyewe kwa wenyewe na pia kupigana na vikosi vya kitaifa na vikosi vya Ufaransa. Juhudi za kupambana na zimefanikiwa kuwaondowa na kusambaratisha baadhi ya shughuli za wanamgambo hao. Lakini hali bado haijaonesha dalili ya kuimarika. Rais wa Mali aliwatuma baadhi ya wajumbe kukutana na kiongozi wa kundi hilo la wanamgambo wa kiislamu la GSIM, Iyad Ag Ghaly na Amadou Koufa kiongozi wa kundi jingine la Katiba Macina.