1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMalawi

Malawi iko hatarini kushuhudia ongezeko la kipindupindu

21 Machi 2023

Malawi inakabiliwa na hatari ya kushuhudia ongezeko la visa vya maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu kufuatia kimbunga Freddy.

https://p.dw.com/p/4Oyhl
Malawi | Zyklon Freddy
Picha: Esa Alexander/REUTERS

Kimbunga Freddy kilisababisha uharibifu mkubwa wa miundo mbinu ya maji na vyoo katika nchi hiyo.

Hayo yameelezwa na wizara ya afya jana jumatatu wakati ikitowa tahadhari.Nchi hiyo tayari ilikuwa ikipambana na mripuko wa ugonjwa huo hatari  wakati kimbunga hicho kilipopiga wiki iliyopita.

Soma pia: Malawi yatoa wito wa msaada wa kimataifa kufuatia kimbunga Freddy

Mripuko huo  ulioanza mwaka jana umeshawathiri zaidi ya watu 30,600 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 1,700.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW