1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIran

Makundi ya Haki: Iran imezuia kumbukumbu ya kifo cha Mahsa

16 Septemba 2023

Makundi ya Haki za Binadamu yamesema mamlaka za Iran zimeizuia familia ya Mahsa Amini, kufanya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kifo cha binti wao ambacho kilizusha wimbi la maandamano nchini humo.

https://p.dw.com/p/4WQLW
Mahsa Amini
Mahsa Amini Picha: DW

Mashirika mawili ambayo ni Mtandao wa Haki za Binadamu wa jimbo la Kurdistan (KHRN) na lile la Haki za Binadamu la Iran lenye makao yake nchini Norway yamesema Baba wa Mahsa alikamatwa na maafisa wa usalama na kisha kuachiwa ndani ya muda mfupi baada ya kuonywa kutofanya mkusanyiko wowote wa kumbukumbu ya kifo cha binti yake.

Polisi pia imeweka vizuizi kwenye makaburi ya alikozikwa msichana huyo kuzuia watu kuyafikia.

Mahsa Amini, binti wa Kiirani mwenye asili ya Kikurdi alipoteza maisha mnamo Septemba 16 mwaka jana akiwa mikononi mwa polisi wa maadili waliomkamata kwa madai ya kukiuka utaratibu wa kuvaa hijabu.

Kifo chake kilizusha ghadhabu ndani ya Iran iliyoshuhudia ghasia za wiki kadhaa zilizodhibitiwa kwa mkono wa chuma na vikosi vya usalama.