1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makumbusho ya maafa Rwanda yaongezwa katika Turathi za Dunia

20 Septemba 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya elimu, sayansi na Utamaduni, UNESCO limeyaingiza makumbusho manne ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda kwenye orodha ya Turathi za Dunia.

https://p.dw.com/p/4Wbbg
Rwanda inakadiria kuwa watu 1,000,050 waliuawa kwenye machafuko hayo ya kikabila ya mwaka 1994.
Rwanda inakadiria kuwa watu 1,000,050 waliuawa kwenye machafuko hayo ya kikabila ya mwaka 1994.Picha: Ben Curtis/AP/picture alliance

UNESCO limeandika kwenye mtandao wa X kwamba makumbusho hayo ni ya Nyamata, Murambi, Gisozi na Bisesero na yanayobeba kumbukumbu ya mauaji ya karibu Watutsi 800,000 pamoja na Wahutu waliokuwa na misimamo ya wastani kati ya mwezi Aprili na Julai 1994.

Makumbusho hayo yamesheheni mafuvu ya vichwa, vipande vya mifupa, nguo zilizochanika na picha za maiti zlizorundikana zimekuwa zikiibua hisia kali kwa wageni wanaotembelea makumbusho ya Gisozi, mjini Kigali ambako kulihifadhiwa wahanga wa karibu 250,000 wa mwisho wa mauaji hayo ya kimbari.