1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makombora yawauwa watu wanne Kherson

21 Oktoba 2022

Nchini Ukraine watu wanne wameuwawa baada ya kushambuliwa na roketi katika eneo la kivuko la Ukraine, lenye kudhibitiwa na Urusi la Kherson.

https://p.dw.com/p/4IVqH
Ukraine Krieg | Russischer Drohnenangriff auf Kiew
Picha: Vladyslav Musiienko/REUTERS

Taarifa za mauwaji hayo zimetolewa na naibu gavana wa mji huo wa Kherson Kirill Stremousov, ambae ameteuliwa na Urusi. zaidi anasema "Jana Oktoba 20, jeshi la Ukraine limekishambulia kivuko cha Kherson. Matokeo ya mashambulizi hayo ni vifo vya watu wanne. Walifyatua makombora kwa maeneo tofauti kwa lengo la kuwauwa watu wengi itakavyowezekana. Na takriban magari 10 ya raia yameteketea."

Hata hivyo upande wa Ukraine umejitenga na kuhusika na shambulizi hilo. Msemaji wa Jeshi la Ukraine,  Nataliya Gumenyuk amesema hawawezi kushambulia miundombinu muhimu na wala hawawezi kuyashambulia makazi tulivu.

Zaidi ya watu 50,000 kuhamishwa Kherson

Mamlaka katika eneo ambalo Urusi ilitangaza kulinyakua mwezi uliopita imesema kwa juma hili wamepanga kuwahamisha kati ya wakazi 50,000 hadi 60,000 katika siku sita zijazo huku likiendelea kuabliwa na mashambulizi ya kuukomboa mjui huo kutoka kwa Ukraine.

Na Rais Volodymyr Zelensky Ukraine ametoa onyo kwamba Urusi inapanga kukiripua bwawa la kuzalisha umeme la Kakhovka katika mji huohuo wa Kherson, ambao vikisi vya Ukraine kwa wakati huu vinaenelezwa kusonga mbele katika mapigano yao. Katika hotuba yake kwa njia ya video kwa viongozi wa Umoja wa Ulaya Zelensky amesema " Urusi inaunda mazingira ya makusudi ya kufanya maafa makubwa kwa watu wa Ukraine."

Hofu ya kuathirika wengi kwa kushambuliwa bwawa la kuzalisha umeme

Ukraine Krieg | Staudamm Kakhovka
Bwawa la kuzalishja umeme la KakhovkaPicha: SNA/IMAGO

Amesema ikiwa kituo hicho kitaripuliwa, kutakuwa na mafuriko makubwa yatakayouthiri mji wa Kherson, hatua ambayo itawaweka katika wakati mgumua maelfu ya watu.

Katika hatua nyingine wizara ya mambo ya nje ya Iran imewataka raia wake kujiepusha na safara za Ukraine lakini pia walipo nchini humo kuondioka mara maoja. Taarifa ya wizara hiyo inasema hatua hiyo inatokana na tofauti za kiusalama baina ya mataifa hayo kwa sasa.

Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje ya mataifa ya Balkan

Hapa Ujerumani Waziri wa Mambo ya Nje, Annalena Baerbock ameonesha nia ya kustawisha ushirikiano wa kikanda katika mkutano wa mataifa ya Magharibi mwa Balkan wa mjini Berlin. Katika mkutano huo mawaziri wa mambo ya nje wa kanda hiyo watajikita katika juhudi ya kuunda soko la pamoja la kikanda. Lakini pamoja na hayo na kwa hali ilivyo sasa suala la uhakika wa upatikanaji wa nishati litapewa nafasi kubwa kutokana na vita kati ya Ukraine na Urusi.

Soma zaidi: Urusi yaionya UN dhidi ya uchunguzi wa ndege za Iran Ukraine

Mkutano huo wenye kutarajiwa kuhudhuriwa na mawaziri wa mambo ya kigeni, unayahusisha mataifa ya Kosovo, Macedonia Kaskazini, Montenegro, na Serbia. Bulgaria, Ugiriki, Austria, Croatia, Slovenia na Jamhuri ya  Czech.

Vyanzo: DPA/RTA/AFP