1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vijiji 5 vya Urusi vyakosa umeme kwa mashambulizi ya Ukraine

29 Aprili 2023

Vijiji vitano vya Urusi kwenye mpaka wake na Ukraine havina umeme kutokana na mashambulizi ya makombora ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4QiNZ
Ukraine Krieg | Brennendes Treibstofflager in Sewastopol
Picha: Karina Sapunova/TASS/dpa/picture alliance

Vijiji vitano vya Urusi kwenye mpaka wake na Ukraine havina umeme kutokana na mashambulizi ya makombora ya Ukrainehiyo ni kwa mujibu wa gavana wa jimbo la Belgorod kusini-magharibi mwa Urusi ambalo linapakana na Ukraine.Kupitia ukurasa wake wa telegram gavana huyo Vyacheslav Gladkov amekitaja kijiji cha Novaya Tavolzhanka kuwa kimeshambuliwa na makombora ya Ukraine leo hii. Miundombinu ya umeme imeharibika huku akiongeza kuwa wakazi katika kijiji hicho na vingine vinne wamesalia gizani.Hata hivyo, Gavana Gladkov amesema taarifa za awali zinaeleza kuwa hakuna mtu aliyeathiriwa. Kimsingi eneo hilo limekumbwa na mashambulizi katika muda wote wa mashambulizi ya Moscow ya zaidi ya mwaka mzima nchini Ukraine.