1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAKISIO YA UMOJA WA ULAYA JUU YA UCHUMI UJERUMANI

5 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CEG5

Uchambuzi wa wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo umetuwama juu ya mada mbili:Ripoti ya majira ya kwanza ya mwaka huu ya Umoja wa Ulaya inayobashiri uchumi wa Ujerumani utakua kidogo tu 2005 na mvutano unaoendelea katika wizara ya nje ya Ujerumani kumhusu waziri wa nje Joshka Fischer.

Ujerumani yadhihirika kwa mwaka wa 4 mfululizo itakiuka mapatano ya kuimarisha sarafu ya Umoja wa Ulaya-Euro.Kujumuishwa lakini kwa Ujerumani Mashariki ndani ya umoja wa Ulaya kungefaa kuikinga Ujerumani kutopewa adhabu kali katikakwa madhambi hayo.

Gazeti la OSTSEE-ZEITUNG lauliza:

Ujerumani mashariki sasa ndio pingamizi kwa maenedeleo ya Ujerumani ?

Alhamisi iliopita,lakumbusha gazeti, ulichomoza mpango mopya wa kuiendeleza mashariki wakati wa mkutano wa miradi mipya ulioitishwa na Shirikisho la wanaviwanda la Ujerumani .Miradi kama hii mingi iliotangulia bila kuungwamkono na juhudi nyengine,haikuchangia kuufufua uchumi.Yote hayo haitasaidia kitu-wajerumani wanahitaji kwa pamoja kujikomboa kutoka msukosuko wa sasa-lausia OSTSEE-ZEITUNG.

Ama gazeti la OSTTHÜRINGER ZEITUNG linalochapishwa mjini Gera laandika:

"Makisio ya majira ya kwanza ya mwaka yaliotolewa na UU yanamurika sura mbaya katika tafsiri mpya ilioafikiwa karibuni katika mapatano ya kuimarisha sarafu ya Euro.Kwani, kutokana na shinikizo na mbinu mbali mbali za kidiplomasia, serikali ya Ujerumani ilifaulu mwishoni mwa mwezi Machi, kuwa kuikukwa mpaka wa nakisi uliowekwa ,kusiadhibniwe mno.Siku chache baadae, sasa, hayo yaliopigiwa makofi kuwa ni mageuzi katika kanuni za bajeti za UM ni kama yale hasa aliotamani waziri wa fedha wa Ujerumani Bw.Eichel................Makisio ya majira ya kwanza ya mwaka ya UU kwa jicho la nchi nyengine zanachama wa UM ,kugeuka pia ni jambo la kuzitia shime."-Hilo lilikua OSTTHÜRINGER ZEITUNG.

Gazeti la PFORZHEIMER ZEITUNG linahisi:

"Mwanya wa maendeleo ya ukuaji uchumi kati ya Ujerumani ya zamani iliokua ikipigiwa mfano na jirani zake unazidi kupanuka na kustusha.H aitoshi hapo kutoa lawama juu ya nguvu za sarafau ya Euro kuathiri biashara ya n’gambo au kupanda mno kwa bei ya mafuta kama ni kisingizio cha hali hiyo.

Kwani nchi nyingi za UU pia zimeathiriwa na hali hiyo.Kizingiti hasa na kikubwa kinachozorotesha ukuaji wa uchumi wa Ujerumani kinasalia kuwa udhaifu wa kuchangamka kwa soko lake la ndani."

Nalo gazeti la KÖLNISCHE RUNDSCHAU laandika kwamba, hata mwaka 2005 dola kuu la kiuchumi la UU limegeuka kutoka mwanafunzi wa kupigiwa mfano na kuwa mgonjwa wa kuuguzwa.Hakuna katika nchi nyengine yoyote ya UU bajeti ya taifa mara kwa mara kubidi kugharimiwa na madeni kama ilivyo Ujerumani.Bila ya shaka tarakimu ya ripoti ya UU ni makisio tu na yamkinika mwaka ukiendelea sura ikatengenea,lakini hakuna matumaini hayo mema .Alao sio kwa jicho la Brussels,kwani berlin haioneshi inaelewa barabara matatizo inayokumbana nayo.

Gazeti la NÜREMBERGER ZEITUNG linatugeuzia mada likichambua mkasa wa waziri wa nje Joshka Fischer:Laandika:

"Fischer amepatwa na mkosi.Alitaka kulisaifisha gazeti linalochapishwa na wizara yake lisiwe na madoa ya rangi ya kahawia na sasa amewaudhi nusu ya watumishi wa wizara yake.Alitaka kwa kurahisisha utoaji viza kwa wale waliotaka kuja Ujerumani, kuondosha mipaka iliojengwa ulaya na mapema na sasa jina lake binafsi limeingia doa na pengine karibuni pia atapoteza wadhifa wake. Haistaajabishi kujikuta amezingirwa na maadui pande zote.Adui yake mkubwa ni ‘mzee rukhsa Joshka Fischer."

Ama likitumalizia uchambuzi huu leo, gazeti la BERLINER ZEITUNG laandika:

"wajerumani walimthamini mwanasiasa Joshka Fischer ambae kwa kweli, hakuwa mwanasiasa.Fischer alibakia kuwa kama alivyo: Fischer halisi.Alikua mwalimu aliejielimisha mwenyewe.Sasa nini awasikilize wasemayo wengine....... wajerumani sasa wana mwanasiasa ambae ni tofauti kabisa na wengine na wanajionea matokeo yake ."