1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makanda wawili wa Urusi wauwawa Ukraine

14 Mei 2023

Urusi inasema kwamba makamanda wake wawili wa kijeshi wameuawa katika mapigano karibu na eneo la mapambano la Bakhmut huko mashariki mwa Ukraine

https://p.dw.com/p/4RL0P
Ukraine Bakhmut Frontline Ukrainische Soldaten
Picha: Sergey Shestak/AFP/Getty Images

Katika tangazo la nadra kuhusu athari wanazozipata katika eneo la vita, wizara ya ulinzi ya taifa hilo imesema kamanda wa kikosi namba nne cha magari ya mashambulizi, Vyacheslav Makarov, na mwininge Yevgeny Brovko, ambaye ni naibu mwenye kuhusika na kazi za siasa jeshini wameuwawa katika mapigano mashariki mwa Ukraine.Tangazo hilo linatolewa katika kipindi ambacho mapigano ya kutaka udhibiti wa Bakhmut katika eneo la mashariki la Donetsk yanaendelea. Wizara ya Ulinzi imesema Kanali Makarov aliuawa wakati kikosi chake kikiwa katika juhudi ya kuyazima mashambulizi ya wanajeshi wa Ukraine kusini mwa maneno ya Krasne.Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu alisema mwaka uliopita wanajeshi 5,937 wa Urusi waliuawa katika mapigano nchini Ukraine ingawa wachambuzi wa kijeshi wanasema Moscow inajaribu kuficha ukubwa wa hasara zake katika vita hivyo.