1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makamu wa Rais wa Marekani kuanza ziara yake barani Afrika

24 Machi 2023

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris anaanza ziara ziara yake ya wiki nzima barani Afrika mwishoni mwa wiki hii.

https://p.dw.com/p/4PBVG
USA Kamala Harris Afrika-Gipfel
Picha: Andrew Harnik/AP Photo/picture alliance

Ziara hiyo inajiri wakati ambapo Marekani ikitaka kujionesha kama mshirika bora kuliko China kwa bara hilo. Makamu huyo wa rais wa Marekani atafanya majadiliano kuhusu kujiingiza kwa China katika masuala ya teknolojia na uchumi barani humo, hatua ambayo inaipa wasiwasi nchi yake.

Marekani pia inakhofia kujiingiza kwa nchi hiyo ya Asia yenye nguvu katika suala la kufanya mabadiliko ya mfumo wa ulipaji  madeni kwa  nchi za Kiafrika.

Soma pia: Biden: Afrika inastahili dhima kubwa zaidi duniani

Moja wa nchi ambazo Kamala Harris atazitembelea ni Zambia ambayo ni ya kwanza katika bara hilo kutangazwa muflisi na kushindwa kulipa madeni yake ya nje wakati wa kipindi cha janga la korona, na iko kwenye mazungumzo na wakopeshaji wake ikiwemo China, kufikia makubaliano.

Kamala Harris atakwenda pia Ghana na Tanzania. Rais wa Marekani Joe Biden nae  pia anatarajiwa kulizuru bara hilo mwishoni mwa mwaka huu.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW