1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makamu wa rais wa Marekani aelekea Tanzania

Daniel Gakuba
29 Machi 2023

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania, kituo cha pili cha ziara yake ya kwanza barani Afrika iliyoanzia nchini Ghana.

https://p.dw.com/p/4PQHx
Ghana | US Vize Präsidentin Kamala Harris in Accra
Picha: NIPAH DENNIS/AFP/Getty Images

Hapo jana kiongozi huyo alifanya ziara katika jengo lililokuwa lango la kuwapitisha watumwa wanaosafirishwa kutoka Afrika kwenda bara Amerika na visiwa vya Karibeani, lililo katika mji wa mwambao wa Cape Coast nchini Ghana. Jengo hilo limewekwa katika orodha ya turathi za dunia. Kamala Harris aliweka shada la maua kwa heshima ya watu waliopoteza maisha katika biashara ya watumwa na kusema kuwa historia hiyo inapaswa kufundishwa nchini Marekani. Awali alikuwa ametoa wito wa uwekezaji zaidi katika sekta ya uvumbuzi barani Afrika huku akielezea matumaini makubwa kwa mustakabali wa bara hilo. Kituo cha mwisho cha ziara hii ya Kamala Harris barani Afrika kitakuwa nchini Zambia.