1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaUjerumani

Makampuni ya Ujerumani yalenga kuwekeza zaidi Afrika

28 Desemba 2022

Makampuni ya Ujerumani yanataka kukuza shughuli zao barani Afrika mwaka ujao, haswa katika maeneo ya gesi ya haidrogeni ambayo haichafui mazingira na gesi iliyosindikwa.

https://p.dw.com/p/4LTkU
Großbritannien | LNG-Gasterminal
Picha: K. Fitzmaurice-Brown/blickwinkel/picture alliance

Haya ni kwa mujibu wa uchunguzi ulionekana na shirika la habari la Reuters. Kura ya maoni ya wanachama wa Muungano wa biashara wa Ujerumani na Afrika imeonyesha kuwa zaidi ya asilimia 39 ya wanachama wa muungano huo wanalenga kuimarisha viwango vyao vya matumizi ya uwekezaji barani Afrika. Soma  Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz yuko Saudi Arabia kusaka nishati kwenye nchi za Ghuba 

Christoph Kannegiesser mkurugenzi wa muungano huo amesema makampuni mengi ya Ujerumani yanataka kupanua shughuli zao mwaka ujao kwasababu bara hilo lipo katika njia ya ukuaji.

soma Uhaba wa nishati: Wajerumani wataka serikali kusaidia

Kulingana na takwimu za wizara ya uchumi makampuni ya Ujerumani yaliwekeza takriban euro bilioni 1.6 barani Afrika mnamo 2021, ambapo takriban euro bilioni 1.1 zilienda kusini mwa Sahara.

Nigeria | Gas Pipeline
Picha: Florian Plaucheur/AFP/Getty Images

Kannegiesser ameongeza kusema kwamba Ujerumani nchi yenye uchumi mkubwa barani Ulaya imekuwa ikitafuta kupunguza utegemezi wake kwa gesi ya Urusi tangu uvamizi nchiniUkraine, na anaona fursa kubwa katika sekta ya nishati barani Afrika.

Kuhusu haidrojeni isiyochafua mazingira na gesi iliyochakatwa kuwa ya kimiminika, amezitaja Senegal, Nigeria, Mauritania na Namibia kama nchi zenye uwezo wa kutoa nishati hizo.

Utafiti huo ulionyesha kuwa asilimia 56 ya kampuni zilitazama shughuli zao biashara barani Afrika mnamo 2022 kuwa chanya na zaidi ya asilimia 7 walisema zilikuwa "nzuri sana".

Muungano huo ambao unasema unawakilisha karibu asilimia 85 ya Biashara za Ujerumani zinazofanya kazi barani Afrika, unataka serikali kutoa msaada kupitia kuboreshwa kwa bima ya mikopo ya nje na dhamana ya uwekezaji kutoka kwa serikali ya Ujerumani ili kuhakikisha biashara barani Afrika haiachiwi Marekani na China.

Aidha muungano huo umekosoa sheria ya Ujerumani inayoanza kutekelezwa Januari 1 ambayo inayalazimu makampuni makubwa kuchukua hatua dhidi ya haki za binadamu na ukiukaji wa hali ya hewa, wakisema haina tija na inaunda safu mpya ya urasimu.