1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makala Maalum : Mfumo mpya wa tovuti.

Matt Hermann/Mohamed Dahman25 Juni 2007

Larry Sanger anahusiana na maarifa matupu.Shahada zake za taaluma ni juu ya epistemolojia elimu ya ufahamu,maisha yake ya kikazi yamekuwa yakihama kutoka tovuti moja ya ensaiklopidia ya seti ya taarifa juu ya mambo mengi kwenda nyengine.

https://p.dw.com/p/CHkQ
Mawasiliano kwa njia ya mtandao.
Mawasiliano kwa njia ya mtandao.Picha: picture-alliance/dpa

Matt Hermann wa Radio Deutsche Welle amezungumza na Larry Sanger juu ya mustakbali wa miradi shirikishi kwenye tovuti na juu ya maoni yake kwamba utaalamu una dhima ya kutimiza kwenye miradi hiyo.

Sanger kwanza alikuwa mhariri mkuu wa tovuti ya Nupedia ya wasomi yenye msimamo wa wastani baadae akawa kwenye tovuti shirikishi ya msimamo mkali ya wikipedia na hivi sasa yuko kwenye tovuti yake mpya ya Citizendium.

Juu ya kwamba Sanger hivi sasa ametingwa na tovuti hiyo ya Citizendium ambayo anatumai kukusanya pamoja donge la wasomi na uadilifu wa wanazuoni katika masuala magumu au tete ambayo tovuti ya wikipedia mara nyingi huyumba katika kuyashughulikia anasema kuna mengi ya kubakia kwenye seti ya tovuti hiyo inayotowa taarifa kuhusu mambo mengi.

(O-TON Sanger)

Nafikiri ni jambo safi sana kuweza kufikia hatua ya kuwaandaa watu ambayo inaruhusu watu kuchangia katika maarifa ya dunia nadhani tu tunahitaji hivi sasa kuingia hatua nyengine kwa kuwawezesha wale waliochunguza hasa masuala hayo kuwa na usimamizi juu ya masuala fulani na bila ya kubadili mfumo ambao wikipedia inafanya kazi.

Kile anachokifikiria Sanger kimeweza kufanya kazi ambayo ni kanuni ya msingi ya wikipedia : matumizi yanayoruhusu waandishi mbali mbali kuhariri ukurasa huo huo au makala.Uzoefu wake umepelekea kuanzishwa kwa mradi wa Nupedia,seti nyengine inayotowa taarifa ya mambo mengi kwenye tovuti ambayo huandikwa na wanazuoni ambayo ilimchachisha kwenye mchakato huo wa jadi wa uhariri wenye mwendo wa pole mno na wa matabaka ya madaraka.Tovuti ya Citizendium inajaribu kwenda kwa haraka.

(O-TON Sanger)

Angalia sisi ni wikipedia hakuna haja ya kukabidhiwa mada wahariri hawatowi maagizo nani wa kushughulikia mada hawalazimiki kuidhinisha makala na kuipeleka kutoka hatua moja kwenda nyengine na kadhalika.Hakuna dhima ya udhibiti ni dhima ya ushiriki wa bega kwa bega lakini wana mamlaka ya kuidhinisha makala na mamlaka ya kutowa maamuzi juu ya makala wakati maamuzi yanapotakiwa kutolewa.Lakini kwa kiasi kikubwa wahariri wanafanya kazi sambamba na watu wasiokuwa wahariri au waandishi.

Hatua nyengine ambayo Citizendium imechukuwa na ambayo Sanger anaamini kuwa ni muhimu ni kusistiza kwamba washiriki wanatumia majina yao halisi wakati wote.Jambo hilo huenda likaondowa ushujaa fulani wa mtandao lakini anasema hufanya mchakato wa uhariri kuwa wa kuwajibika zaidi na wa urafiki.

(O-TON Sanger)

Siwezi kuwa na furaha kupindukia hii kutokana na matokeo ya sera hiyo.Ilikuwa ni jambo zuri kuangalia mabadiliko ya hivi karibuni kwenye tovuti ya Citizendium na kuona majina halisi ya watu.Unapata wazo kwamba unawasiliana na watu ambao unawajuwa au angalau unaweza kuwajuwa. Na huleta uhai kwenye tovuti hiyo na na kufanya ushiriki uwe rahisi zaidi.

Je Lawrence Mark Larry Sanger ambalo ni jina lake halisi yuko tayari kujiita mtaalamu na kusimamia baadhi ya makala kwenye tovuti yake?

Jibu lake ni kwamba yumkini akawa ni mtaalamu wa kuhusu jumuiya za mtandao lakini utaalamu wake unahusu tu kile anachofanya na kufikiria kile anachofanya.