1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makaburi ya wengi yagunduliwa Libya

12 Juni 2020

Umoja wa Mataifa umeonesha uwepo wa hali ya kitisho nchini Libya baada ya taarifa zilizobaini uwepo wa makaburi manane ya watu wengi, katika eneo ambalo liliweza kudhibitiwa na serikali ya kitaifa.

https://p.dw.com/p/3dfZG
Libyen, Tripoli: Übernahme des Flughafens
Picha: picture-alliance/H. Turkia

Makaburi hayo yamegunduliwa katika maeneo yaliyokuwa yakidhibitiwa na vikosi vya serikali ya kitaifa wakati wa makabiliano, baada ya vikosi vya mbabe wa kivita Khalifa Haftar kuondoka katika eneo hilo.

Taarifa ya mpango wa ulinzi wa amani nchini Libya (UNSMIL) inasema makaburi hayo yamebanika katika eneo la Tarhuna, kusini mashariki mwa mji mkuu Tripoli, siku chache zilizopita.

Aidha taarifa hiyo imeongeza kwa kusema "sheria ya kimataifa inaitaka mamlaka kufanya uchunguzi madhubuti na wa haraka, wenye uwazi ili kuwafikisha katika mikono ya sheria wale wote waliohusika na mauwaji." Makaburi kadhaa ya watu wengi yamegunduliwa katika maeneo ya karibu na Tarhuna tangu eneo hilo litiwe mikononi mwa serikali inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.

Mwandishi wa shirika la habari la Ufaransa AFP alipata nafasi ya kufika katika eneo ambalo miili kadhaa ya watu ilifukuliwa na Shirika la Hilali Nyekundu kwa ajili ya utambuzi.