Majeshi ya usalama Sudan yapambana na waandamanaji
20 Desemba 2018Matangazo
Majeshi ya usalama yamefyatua mabomu ya kutoa machozi baada ya mamia ya waandamanaji kuingia mitani katika kitongoji cha mji wa Atbara nchini Sudan leo, wakiimba nyimbo za kuipinga serikali.
Hali ya hatari imetangazwa katika mji huo jana baada ya mamia ya watu kuandamana dhidi ya ongezeko la bei na kuchoma moto makao makuu ya chama tawala katika eneo hilo.