1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majeshi ya Israel yakaribia kuingia Gaza City

2 Novemba 2023

Majeshi ya Israel leo yameendelea kuingia Gaza City ila yamekumbana na upinzani mkali kutoka kwa wanamgambo wa Hamas waliowashambulia kwa makombora na mashambulizi ya kushtukiza kutoka kwenye mahandaki.

https://p.dw.com/p/4YJKK
Baadhi ya wanajeshi wa Israel wakiwa karibu na mpaka wa Israel na Gaza
Baadhi ya wanajeshi wa Israel wakiwa karibu na mpaka wa Israel na Gaza Picha: Middle East Images/ABACA/picture alliance

Kamanda wa jeshi la Israel Brigedia Jenerali Itzik Choen amesema jeshi lake "lipo katika mlango wa Gaza City."

Ushuhuda wa wakaazi na video kutoka makundi ya Hamas na Islamic Jihad, zimewaonyesha wapiganaji wa makundi hayo wakitokea kwenye mahandaki na kurusha makombora na kisha wakirudi ndani ya mtandao huo wa mahandaki.

Mamia ya raia wa kigeni waingia Misri kutokea Gaza

Wakati huo huo, Saudi Arabia leo imesema inaanzisha kampeni ya ufadhili wa Wapalestina walioko Gaza, ambapo Israel inafanya operesheni ya kijeshi kufuatia mashambulizi ya Hamas ya Oktoba 7.

Chombo cha habari cha Al-Ekhbariya huko Saudi Arabia kimeripoti kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman ametoa mchango wa dola milioni 5.3 katika kampeni hiyo.