1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSaudi Arabia

Mahujaji waelekea Arafat, wengine wajiandaa kwa Eid al-Adha

15 Juni 2024

Mamilioni ya Waislamu duniani wanajitayarisha kwa sherehe za sikukuu ya Eid al-Adha zitakazofanyika kesho, ikiwa ni ishara ya kukamilika kwa ibada ya Hijja kwenye mji mtakatifu wa Makkah nchini Saudi Arabia.

https://p.dw.com/p/4h48a
Mahujaji wa Kiislamu wakishiriki ibada ya Hijja ya mwaka 2024.
Mahujaji wa Kiislamu wakishiriki ibada ya Hijja ya mwaka 2024. Picha: Rafiq Maqbool/AP Photo/picture alliance

Hii leo mamia kwa maelfu ya mahujaji watakusanyika kwa ibada katika eneo la mlima Arafat ikiwa ni kilele cha Hija ambayo ni moja ya nguzo kuu tano za dini ya Uislamu.

Wakiwa kwenye mlima huo ambao inakoaminika Mtume Muhammad (S.A.W) alitoa hotuba ya mwisho kwa umma wa Waislamu kiasi miaka 1,400 iliyopita, waumini wataomba dua na kufanya toba kwa Mwenyezi Mungu. 

Hapo jana licha ya hali ya joto kali, waumini hao walianza ibada ya Hijja kwenye eneo la jangwa la Mina nje kidogo ya mji mtakatifu wa Makkah.

Kesho jumapili mahujaji watashiriki tukio la ishara la kumpiga mawe shetani wakati waumini wengine ulimwenguni wakisheherekea sikukuu ya Eid inayojumisha uchinjaji wa wanyama.