1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahasimu Sudan kusitisha vita kwa siku saba

21 Mei 2023

Mahasimu Sudan kusitisha vita kwa siku saba

https://p.dw.com/p/4Rd5E
Sudan Unruhe Konflikt
Picha: AFP via Getty Images

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya Marekani, mahasimu hao kwa mara ya kwanza wamefanya makubaliano hayo na kuweka sahihi zao.Kwa Taarifa iliyotolewa Jumamosi jioni imesema kwamba makubaliano hayo  ya kuweka chini silaha yaliyofanyika mjini Jeddah Saudi Arabia, yanakusudia kuwapa watu wa Sudan nafasi ya kupata misaada ya kiutu. Mazungumzo ya kusimamisha mapigano kati ya jeshi la Sudan linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattahal-Burhan, dhidi ya kikosi cha dharura cha RSF kinachoongozwa na Hamdan Daglo yanasimamiwa na Marekani pamoja na Saudi Arabia.Mzozo wa kugombea madaraka kati ya jeshi la Sudan na kundi la RSF yameitumbukiza Sudan ndani ya mzozo mkubwa wa kibinadamu uliowalazimisha zaidi ya watu milioni 1.1 kukimbia makwao ikiwemo kuingia kwenye mataifa jirani.