1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahama kuwania tena urais wa Ghana

14 Mei 2023

Chama kikuu cha upinzani nchini Ghana, National Democratic Congress, kimemchagua tena kwa wingi wa kura rais wa zamani, John Mahama, kuwa mpeperusha bendera wake kwa uchaguzi wa rais wa 2024.

https://p.dw.com/p/4RKDd
Afrika Ghana Präsidentschaftswahlen  John Dramani Mahama
Picha: Nipah Dennis/AFP/Getty Images

Kamati iliyohusika na uchaguzi huo wa ndani ilisema Mahama mwenye umri wa miaka 64, alipata jumla ya kura 297,603, sawa na asilimia 98.9 ya kura zilizopigwa. Hii ni mara ya tatu kwa Mahama kuwania nafasi hiyo ya juu Ghana, mojawapo ya nchi zenye demokrasia imara zaidi barani Afrika. Alipata nafasi ya wa pili katika mchuano wa rais nyuma ya Rais Nana Akufo-Addo katika miaka ya 2016 na 2020. Uchaguzi ujao wa urais, unatarajiwa kuwa wa upinzani mkali. Hakuna chama ambacho kiliwahi kushinda zaidi ya mihula miwili kwa mfululizo na taifa hilo lipo kwenye mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi ambao umechochea ongezeko la gharama za maisha na kusababisha pia sarafu ya taifa hilo "cedi' kuporomoka, hali iliyochangia kuibuka kwa maandamano.