1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mahakama ya Pakistan imetaka Khan afikishwe mahakamani

23 Novemba 2023

Mahakama ya Pakistan leo Alhamisi imetoa maagizo kwa maamlaka za nchi hiyo kumfikisha mahakamani waziri mkuu wa zamani Imran Khan mnamo Novemba 28.

https://p.dw.com/p/4ZLkg

Hayo yameelezwa na wakili wake, katika kile ambacho kitakuwa ni kwa  mara ya kwanza kwa mwanasiasa huyo kuonekana hadharani tangu alipotiwa jela mnamo mwezi Agosti mwaka huu. Mahakama kuu ya mjini Islamabad mwanzoni mwa wiki hii ilitangaza  kwamba kuendeshwa gerezani  kwa  kesi kuhusu mashtaka ya kuvujisha siri za nchi dhidi yaKhan ni kinyume cha sheria.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW