1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikwazo Venezuela ilivyowekewa na EU vyatupiliwa mbali

13 Septemba 2023

Mahakama ya Umoja wa Ulaya nchini Luxenmbourg imefutilia mbali hatua za kisheria zilizochukuliwa na Venezuela kupinga vikwazo ilivyowekewa na Umoja huo wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/4WInP
2020 Luxemburg | Schild und Logo des Gerichtshofs der Europäischen Union
Picha: John Thys/AFP/Getty Images

Majaji wamepitisha uamuzi kwamba hatua za kuiadhibu Venezuela zilizochukuliwa na Umoja wa Ulaya zilikuwa na msingi kutokana na kushuhudiwa, vurugu,matumizi makubwa ya nguvu,ukiukaji wa haki za binadamu pamoja na kitisho kwa demokrasia  nchini humo.

Kwa mujibu wa majaji,kulikuwa na ushahidi wa kutosha wakati Umoja wa Ulaya ulipopitisha vikwazo dhidi ya Venezuela mwaka 2017. 

Nchi hiyo imetowa hoja  kwamba vikwazo vya Umoja wa Ulaya vimetokana na makosa ya kutengenezwa wakati hali ya kisiasa ya nchi hiyo ikipothminiwa.

Venezuela hata hivyo inaweza kuupinga uamuzi wa mahakama ya Luxenmbourg katika mahakama ya juu kabisa ya haki ya Umoja wa Ulaya, ECJ.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW