1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Mahakama ya Juu ya Marekani yamsafishia njia Trump

5 Machi 2024

Mahakama ya Juu nchini Marekani imemsafishia njia rais wa zamani Donald Trump kuwania urais katika uchaguzi ujao baada ya kutoa uamuzi unaoyazuia majimbo ya nchi hiyo kuliondoa jina lake kwenye kura za mchujo.

https://p.dw.com/p/4dALD
Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump Picha: Alon Skuy/AFP/Getty Images

Katika uamuzi huo wa pamoja uliotolewa jana jioni, majaji 9 wa mahakama hiyo wamebatilisha uamuzi wa mahakama kuu ya jimbo la Colorado uliozuia jina la Trump kuwemo katika kura za mchujo za jimbo hilo.

Mnamo Disemba mwa jana Mahakama ya Colorado ilitoa hukumu kwamba Trump hatoruhusiwa kuwania urais kwenye jimbo hilo kwa msingi kwamba alihusika kuchochea uasi dhidi ya serikali mnamo Januari 6 mwaka 2021.

Hata hivyo Mahakama ya Juu imesema majimbo ya Marekani hayana nguvu kisheria ya kuwaondoa wagombea kwenye kinyang ányiro cha uchaguzi. Trump ameutaja uamuzi huo kuwa ushindi mkubwa kwa Marekani.