1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya juu ya Kenya yatengua uamuzi wa sheria ya fedha

20 Agosti 2024

Mahakama ya juu nchini Kenya imeusimamisha uamuzi uliotolewa na mahakama ya ngazi ya chini uliosema kwamba sheria ya fedha ya mwaka 2023 ilikiuka katiba.

https://p.dw.com/p/4jgyi
Rais wa Kenya William Ruto
Rais William Ruto wa Kenya alikabiliwa na pigo baada ya mahakama ya rufani kuamua kuhusu sheria ya fedha ya 2023Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Mahakama hiyo ya juu imesema ni muhimu kudumisha uimara katika bajeti mpaka hapo hoja za rufani za serikali zitakaposikilizwa mwezi ujao.

Miswada ya bajeti inayowasilishwa bungeni kila mwaka ndiyo njia muhimu kwa serikali kupanga hatua za kuingiza mapato ikiwa pamoja na kupandisha kodi.

Hukumu iliyotolewa na mahakama ya rufani mwezi uliopita ilikuwa pigo kwa serikali ya Rais William Ruto ilipoamua kwamba sheria ya bajeti ya mwaka 2023 ilikiuka katiba.

Uamuzi huo ulifuatia hatua ya Serikali ya Kenya ya kuuondoa mswada wa bajeti wa mwaka huu mnamo mwezi wa Juni kutokana na maandamano ya vijana. Rais Ruto amesimama njia panda kati ya matashi ya wananchi na masharti ya mashirika ya mikopo kama vile Shirika la Fedha la kimataifa, IMF.