1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Mahakama ya juu Venezuela yathibitisha ushindi wa Maduro

23 Agosti 2024

Mahakama ya juu nchini Venezuela imeuthibitisha ushindi wa Rais Nicolas Maduro katika uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita licha ya ukosoaji.

https://p.dw.com/p/4jpI0
Venezuela l Rais Nicolas Maduro
Ushindi wa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro aidhinishwa rasmi na mahakama licha ya kuzozaniwaPicha: Matias Delacroix/AP/dpa/picture alliance

Mahakama hiyo imesema hesabu zilizooneshwa na upande wa upinzani kuwa Maduro alishindwa katika uchaguzi huo ni za kupikwa.

Mahakama hiyo kuu nchini Venezuela, imesema imeidhinisha bila ya mashaka yoyote matokeo ya uchaguzi wa tarehe 28 mwezi Julai yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyomtangaza Maduro kuwa mshindi.