1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiKenya

Mahakama ya Juu Kenya yasema Sheria ya Fedha ni halali

30 Oktoba 2024

Mahakama ya Juu nchini Kenya imeubatilisha uamuzi uliotolewa na mahakama ya rufaa ukiifuta sheria ya fedha ya mwaka wa 2023. Maandamano makali mwezi Juni na Julai ya kupinga sheria hiyo yalisababisha vifo vya watu 60.

https://p.dw.com/p/4mNll
Kenya | Hotuba ya William Ruto baada ya maandamano
Serikali ya Ruto, iliyoingia madarakani Septemba 2022, ilitaka kuweka awamu mpya ya nyongeza ya kodi mwaka huuPicha: atrick Ngugi/AP Photo/picture alliance

Hatua hiyo ni ushindi kwa serikali baada ya maandamano yaliyomlazimu Rais William Ruto kuondoa mswada wa fedha wa mwaka huu. Mahakama ya Juu imesema katika uamuzi wake kuwa imeuweka kando uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ulioitangaza Sheria yote ya Fedha ya 2023 kuwa kinyume na katiba.

Serikali ya Ruto, iliyoingia madarakani Septemba 2022, ilitaka kuweka awamu mpya ya nyongeza ya kodi mwaka huu. Hatua hiyo iliwakasirisha raia wengi na kusababisha maandamano makali mwezi Juni na Julaiambapo zaidi ya watu 60 waliuawa.

Ruto anahoji kuwa nyongeza ya kodi ni muhimu kusaidia kufadhili miradi ya maendeleo nchini Kenya na kulipia mzigo mkubwa wa deni la umma.