1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiUlaya

ICJ yaitupilia mbali kesi ya Ukraine dhidi ya Urusi

1 Februari 2024

Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ imeikataa kwa sehemu kubwa kesi ya mwaka 2017 ya Ukraine iliyoituhumu Urusi kwa kufadhili ugaidi kwa kuwaunga mkono waasi wanaoiunga mkono Moscow mashariki mwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4buUm
The Hague, Uholanzi | Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ
Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ wakiendesha kesiPicha: Remko de Waal/ANP/AFP/Getty Images

Majaji wa mahakama hiyo pia kwa sehemu kubwa wameyatupilia mbali madai ya ubaguzi dhidi ya Waukraine katika eneo la Donbass na Tatars huko Crimea, ikisema hakuna ushahidi wa kutoshakuthibitisha madai hayo ya Ukraine.

Zaidi ya hayo, ombi la Ukraine la kutaka Urusi ilipe fidia, limekataliwa. Uamuzi huo unaashiria kushindwa kwa Ukraine ambayo ilikuwa inatarajia kutumia ushindi wa kisheria katika kesi hiyo kushinikiza vikwazo zaidi dhidi ya Urusi.

Soma pia:Viongozi wa Umoja wa Ulaya wahimizana juu ya kuongeza misaada kwa Ukraine

Ila majaji walisema kwamba Urusi ilikwenda kinyume na uamuzi wake wa muda wa mwaka 2017 uliozitaka pande hizo mbili kufanya kila mbinu kuzuia kuenea kwa mzozo huo.