1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAzerbaijan

ICJ: Azerbaijan kuhakikisha usalama wa Waarmenia Karabakh

18 Novemba 2023

Mahakama ya (ICJ) imetoa agizo la kuitaka Azerbaijan kuhakikisha usalama wa watu wa Armenia wanaoondoka ama wanaotaka kubaki katika eneo la Nagorno Karabakh

https://p.dw.com/p/4Z7gg
Rais wa Azerbaijan  Ilham Aliyev  akizungumza katika kongamano moja huko Baku mnamo Oktoba 2, 2023
Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev Picha: Azerbaijani Presidency/AA/picture alliance

Ikijibu agizo hilo la mahakama, wizara ya mambo ya nje ya Azerbaijan, imesisitiza msimamo wa nchi hiyo kwamba haikuwafurusha raia wowote wa Armenia kutoka eneo hilo na kwamba wengi waliondoka licha ya mwito wa serikali wa kuwataka kubaki.

Soma pia:Azerbaijan yapeperusha bendera ya taifa lake Karabakh

Wizara hiyo imeendelea kusema kuwa Azerbaijan imejitolea kuzingatia haki za binadamu za wakazi wa Armenia katika eneo hilo la Karabakh katika misingi ya usawa na raia wengine wa Azerbaijan 

Maagizo hayo ni hatua ya awali ya kesi iliyofunguliwa na Armenia ikiituhumu Arzebaijan kwa kukiuka azimio la kimataifa dhidi ya ubaguzi wa rangi unaohusishwa na Nagorno-Karabakh.