1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya EU yalaani shambulizi la sumu la Urusi la 2020

6 Juni 2023

Mahakama ya haki ya Ulaya imeilaani Urusi kwa kushindwa kuchunguza kikamilifu tukio la mwaka wa 2020 la kupewa sumu kingozi wa upinzani Alexei Navalny ambalo nchi za Magharibi zilisema lilikuwa jaribio la mauaji.

https://p.dw.com/p/4SGdF
Russland | Oppositionsführer Alexej Nawalny
Picha: Yulia Morozova/REUTERS

Mahakama ya haki ya Ulaya imeilaani Urusi kwa kushindwa kuchunguza kikamilifu tukio la mwaka wa 2020 la kupewa sumu kingozi wa upinzani Alexei Navalny ambalo nchi za Magharibi zilisema lilikuwa jaribio la mauaji. Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binaadamu yenye makao makuu yake mjini Strasbourg imesema Urusi ilishindwa kuchunguza madai ya kuwepo uwezekano wa sababu ya kisiasa kwa jaribio hilo la mauaji, pamoja na uwezekano wa kuhusika maafisa wa serikali. Imesema Urusi ilikataa kuanzisha uchunguzi wa uhalifu kuhusiana na shambulizi hilo la sumu, ambalo lilisababisha Navalny kupoteza fahamu na kuwekwa kwenye mashine ya kumsaidia kupumua. Urusi imeamuriwa kumlipa Navalny euro 40,000 kama fidia ya uharibifu. Navalny mwenye umri w amiaka 47 kwa sasa yuko kwenye gereza moja la mkoa wa Vladimir nchini Urusi, huku kukiwa na wasiwasi unaoongezeka kuhusiana na afya wake.