1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mahakama Pakistan yaridhia dhamaa Imran Khan

22 Desemba 2023

Mahakama ya Juu nchini Pakistan leo imeidhinisha dhamana kwa waziri mkuu wa zamani Imran Khan.

https://p.dw.com/p/4aTR0
Imran Khan
Picha: Mohsin Raza/REUTERS

Mahakama ya Juu nchini Pakistan leo imeidhinisha dhamana kwa waziri mkuu wa zamani Imran Khan na mmoja wa wasaidizi wake katika kesi inayohusiana na madai ya kuvujisha siri za serikali.Mmoja wa mawakili wa kiongozi huyo wa zamani Salman Safdar amesema haikuwa wazi iwapo Khan angeachiliwa kutoka gerezani kutokana na kuwepo kwa hati kadhaa za kukamatwa kwake katika kesi nyingine.Imran Khan, nyota wa zamani wa mchezo wa kriketi, amekuwagerezani tangu mwezi Agosti baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya rushwa.Amekanusha mashtaka ya kuvujisha siri za serikali. Kesi hiyo inahusiana na waraka wa siri uliotumwa nyumbani na balozi wa Pakistan nchini Marekani ambao Khan anatuhumiwa kuuweka hadharani.