1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mahakama Pakistan yampa dhamana Nawaz Sharif

Hawa Bihoga
19 Oktoba 2023

Mahakama ya Pakistan imetoa dhamana kwa waziri mkuu wa zamani na mwenye hatia ya ufisadi aliyeko uhamishoni nchini Uingereza, Nawaz Sharif, na kuondoa kitisho cha kukamatwa atakaporejea nchini humo mwishoni mwa juma.

https://p.dw.com/p/4Xk9S
Korruption Pakistan | Ex-Premierminister Nawaz Sharif
Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Nawaz Sharif.Picha: K.M. Chaudary/AP/dpa/picture alliance

Uamuzi huo wa mahakama unamruhusu kurejea katika mji wake wa Lahore siku ya Jumamosi (Oktoba 21), kwa ajili ya mkutano wa kumkaribisha nyumbani ulioandaliwa na chama chake, wakati mpinzani wake mkuu, Imran Khan, akisota gerezani.

Soma zaidi: Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan aondolewa madarakani

Wakili wake, Amjad Pervaiz, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mahakama imempatia mteja wake dhamana ya ulinzi hadi Oktoba 24 na kuongeza kuwa hawezi kukamatwa atapowasili akitokea nchini Uingereza kwa matibabu.

Soma zaidi: Sharif achaguliwa waziri mkuu mpya Pakistan baada ya kuondolewa Khan

Sharif alihudumu kama waziri mkuu katika awamu tatu tafauti na aliondolewa 2017, na kuzuiliwa kujihusisha na siasa maisha yake yote baada ya kupatikana na hatia ya ufisadi.