Mahakama Kuu Uingereza yasikiliza kesi ya Trump
16 Oktoba 2023Mahakama Kuu nchini Uingereza ilianza siku ya Jumatatu (Oktoba 16) kusikiliza kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa rais wa Marekani, Donald Trump, dhidi ya afisa wa zamani wa upelelezi wa Uingereza, Christopher Steele, ambaye alieneza madai kwamba Urusi ilikuwa inafadhili kampeni ya urais ya Trump mwaka 2016.
Soma: Mahakama yamtia hatiani Trump kwa udanganyifu
Taarifa hizo zenye utata ambazo zilizusha mtafaruku wa kisiasa muda mfupi kabla ya kuapishwa kwa Trump mwezi Januari 2017, zilisema pia kuwa Idara ya Usalama ya Urusi (FSB) ilikuwa na video za ngono za Trump wakati wa safari yake ya mwaka 2013 katika mji mkuu wa Urusi, Moscow.
Trump, ambaye amesema pia yuko tayari kutoa ushahidi katika kesi hiyo, amekuwa akikanusha vikali madai hayo na alifunguwa mashitaka dhidi ya Steele na kampuni yake ya ujasusi ya Orbis katika Mahakama Kuu ya Uingereza Novemba 2022.