1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Kenya yaonywa kutumia nguvu kupita kiasi

28 Juni 2024

Mahakama pia imetoa amri ya kuwazuia polisi kufanya mauaji ya kiholela, kuwakamata, kuwaweka kizuizini, kuwanyanyasa, kuwatesa waandamanaji au kuwafanyia vitendo vya ukatili.

https://p.dw.com/p/4heI5
Maandamano ya Nairobi
Polisi wa Kenya wakimburuta mwandamanajiPicha: Monicah Mwangi /REUTERS

Mahakama Kuu nchini Kenya imepiga marufuku maafisa wa polisi kutumia nguvu kupita kiasi kukabiliana na waandamanaji.

Katika uamuzi uliotolewa na jaji Mugure Thande, polisi wamezuiwa pia kutumia maji ya kuwasha, mabomu ya kutoa machozi, risasi za moto na za mpira, ama mbinu nyengine zozote zitakazoonekana kuwa kali dhidi ya waandamanaji.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, uamuzi huo umefuatia kesi ya dharura iliyowasilishwa mahakamani na wakili Saitabao Ole Kanchory. Mahakama ya Kenya yaidhinisha kutuma jeshi huku vijana waandamanaji wakitafakari hatua inayofuata

Mahakama pia imetoa amri ya kuwazuia polisi kufanya mauaji ya kiholela, kuwakamata, kuwaweka kizuizini, kuwanyanyasa, kuwatesa waandamanaji au kuwafanyia vitendo vya ukatili.

Maandamano yaliyoongozwa kwa kiasi kikubwa na vijana yamefanyika wiki hii baada ya bunge la kitaifa kuupitisha mswada tata wa fedha uliotoa mapendekezo ya kuongeza ushuru kwa mkate na mafuta ya kupikia.