Mageuzi ya katiba kuhusu hijabu Uturuki
3 Februari 2008Matangazo
ANKARA:
Maelfu ya watu wameandamana mitaani katika mji mkuu wa Uturuki,Ankara kupinga mpango wa serikali wa kutaka kuwaruhusu wanafunzi wa kike katika vyuo vikuu, kujifunika kichwa kwa vazi la hijabu.Juma lijalo bunge linatazamiwa kuidhinisha mageuzi ya katiba kuhusu amri ya mwaka 1989 iliyopiga marufuku kwa wanafunzi katika vyuo vikuu,kujifunga vitambaa vya kichwani.
Mswada wa mageuzi umependekezwa na chama tawala cha AKP chenye mizizi ya Kiislamu pamoja na chama cha kizalendo cha upinzani.Lakini wale wanaopinga mswada huo wana hofu kuwa mageuzi yaliyopendekezwa,huenda yakahatarisha taifa ambalo serikali yake hutenganisha siasa na masuala yanayohusika na dini.