1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini: Merkel akubaliana na mkataba wa uhamiaji wa UN

Sekione Kitojo
22 Novemba 2018

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamezungumzia zaidi hotuba ya kansela Merkel bungeni,pamoja na matamshi ya rais Trump kwamba anaangalia mikataba ya mauzo ya silaha na Saudi Arabia badala ya ukiukaji wa haki za binadamu

https://p.dw.com/p/38i3d
Deutschland Bundeskanzlerin Angela Merkel im Bundestag
Picha: picture-alliance/dpa/M. Kappeler

Gazeti  la  Frankfurter Allgemeine Zeitung likiandika  kuhusu  mjadala wa  bajeti bungeni  na  hotuba  ya  kansela  Merkel  kuhusu uhamiaji linasema, Merkel  angeweza kulipima vizuri kwa  usawa wa manufaa na madhara  yake  suala  hili, badala  yake  amejiweka katika  kundi la  mataifa  ambayo yanaonekana  kuwa  yanapendelea tu haki  za binadamu. Mhariri  anaandika:

Hii ni  kazi  bure, kwa  kuwa  Merkel  anafikiri yuko  katika  upande wa  watu  wanaotaka  kufanya  mema  zaidi duniani  na  sio wa wale wenye hisia  za  uzalendo  ambao  wanafikiria  wakati  wote  kuhusu mipaka  ya  nchi  zao. Kifungu anachopenda  kunukuu  ni  kifungu cha kwanza  katika  katiba , kwa  kuwa nchi yoyote inayotumia  nguvu dhidi  ya  raia  wake  inapaswa  kuzuiwa  kufanya  hivyo.

Gazeti  la  Mannheimer  Morgen  likiandika  kuhusiana  na  mkataba wa  Umoja  wa  mataifa  kuhusu  wahamiaji  linasema:

Wakati  wahamiaji  katika  nchi  nyingi  wanakotoka  wakitambua kuhusu  masharti  magumu  yanayokumbana  nayo, wasingejaribu kufika  katika  mataifa  tajiri. Ushirikiano , na  wakati  huo  huo misaada , ama  pia  idadi  maalum  ya  wanaoruhusiwa  kuingia  ni suala  linalotiliwa  mkazo  sana  nchini  Ujerumani. Kwa  pamoja  ama mmoja  mmoja, pamoja  na  hayo  maisha katika  kila  familia yanaonesha  ushirikiano  unasaidia.

Gazeti  la Frankenpost  linazungumzia  kuhusu  uhusiano kati  ya rais  Trump  na  viongozi  wa  Saudia. gazeti  linaandika

Rais Trump  amesisitiza  kwamba  Saudia  ni mshirika  muhimu katika  mapambano  dhidi  ya  ugaidi, pamoja  na  utawala  wa  Iran. Lakini kumbukeni kwamba Wamarekani  waliwahi  kuubeba  utawala wa  Shah Reza Pahlevi na  kupuuza hasira za wananchi  wa  Iran waliochukizwa sana. Mhariri  anaandika  kwamba  Wamarekani wanaweza  kuwa  washindwa , wakati  utawala  wa  Riyadh utakapoangushwa  katika  mapinduzi.

Mpambano  kati  ya halmashauri  ya  Umoja  wa  Ulaya  na  serikali ya  Italia ndio  mada  inayojadiliwa  na  mhariri  wa  gazeti  la Landeszeitung. Mhariri  anaadikika:

Mpambano  huo  unaonekana  kuiingiza Ulaya katika  mzozo  wa muda  mrefu. Lakini Umoja  wa  Ulaya  hautaweza  kushinda mpambano  huo dhidi  ya  Italia. Italia  yenye  uchumi  wa  tatu mkubwa  barani  Ulaya  ni  kubwa  mno kuweza  kuokolewa. Umoja wa  Ulaya  unaonesha kwamba  vyama  vya  Lega  na  Nyota  tano vinataka kutumia  suala  hilo  katika  uchaguzi wa  bunge  la  Ulaya. Wakifanikiwa  kunyakua  wingi katika  bunge  hilo, mradi  wa  Ulaya umekufa.

 

Mwandishi : Sekione  Kitojo / inlandspresse

Mhariri: Yusuf, Saumu