1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazeti ya Ujerumani na kifo cha kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni

4 Aprili 2005

Habari juu ya kufariki dunia kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Johanna Paulo wa Pili zimezusha huzuni na msiba kote duniani.Waumini wamekua wakimiminika kwa maelfu makanisani kumsomea Johanna Paulo wa pili .Nchini Ujerumani hali ndio hiyo hiyo.Wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo wamejishughulisha na mwisho wa enzi,maagano na mwanzo wa enzi mpya.

https://p.dw.com/p/CHOE

Gazeti la HAMBURGER MORGENPOST linasema:

"Mapema mwaka 1978,pale Albino Luciani alipochaguliwa kua Johanna Paulo wa kwanza,upepo wa buruda uliiliwaza Vatican iliyokua imezeeka.Wakati ulikua umeshawadia tena!Umati wa waumini walikua na kiu cha majibu kwa masuala chungu nzima yanayoambatana na wakati unaokwenda ukibadilika.Lakini mageuzi na Perestoika ya Vatikan,yaliishia njiani,mchamungu huyo wa kitaliana alipofariki dunia kwa ghafla,siku 99 tuu baada ya kuchaguliwa kuwaongoza waumini wa kanisa katoliki ulimwenguni.Hamu ya mageuzi ilijipatia msukumo wa aina mpya,pale kardinal wa kutoka Poland,alipochaguliwa kwa mshangao wa wengi kukikalia kiti kitakatifu; mwanaspoti,mtu mwenye uso mkunjuvu na tabasamu,mwenye kupenda watoto na mwerevu anapokabiliana na vyombo vya habari.Ilidhihirika kana kwamba Vatikan inaachana na mitindo ya zama za kale.Ilidhihirika tuu lakini…Bila ya kujali chochote Papa huyu amesaidia pakubwa kuwafumbua watu macho dhidi ya ukoministi.Amewatahadharisha watu yanapohusika masuala kama kwa mfano:kinga dhidi ya maradhi ya ukimwi,akipinga moja kwa moja watu kutumuia vipira kwa mfano,ushauri kwa wajawazito wanaotaka kuharibu mimba,ushoga na akaanzisha uhuru wa maoni kanisani.Papa huyo ameibadilisha dunia yetu kwa namna ambayo hata kanisa lake amelisahau.

Gazeti la mjini München ABENDZEITUNG limeandika:

"Ukakamavu wake dhidi ya aina yoyote ya kuchunguza mimba haukua na kifani.Lakini msimamo huo haukua na faida katika kupambana na umasikini na idadi iliyopindukia ya wakaazi wa dunia.Na jinsi alivyokua akilaani jipira, katika wakati ambapo UKIMWI umeshajitokeza kua kitisho kikubwa cha dunia yetu,msimamo huo pia haukusaidia kupunguza hatari ya kutapakaa maradhi hayo.Tukichukua mfano wa upinzani wake katika mageuzi ya ndani kanisani,kuanzia hali ya mchamungu kusalia mtawa hadi kufikia suala la wanawake kupanda daraja kanisani,yote hayo yanatoa picha isiyo ya kuvutia.Lakini mambo kama haya ya kutatanisha ndiyo yanayomfanya azidi kuvutia.Wale wale walioingiwa na hasira alipozungumzia juu ya ubora wa kanisa katoliki kuliko imani zote nyengine,walifurahishwa na msimamo wake dhidi ya vita vya Iraq."

Gazeti la EßLINGER ZEITUNG linaandika:

"Kanisani kwenyewe kuna walikua wakimbisha:Msimamo wake wachamngu waendelee kuwa watawa na dhidi ya wachamngu wa kike kupanda daraja,ushupavu wake linapohusika suala la maadili kati ya mke na mume na jinsi alivyopigania kutengwa mashoga,yote hayo ni mwiba wa mchongoma kwa wapenda mageuzi waliokua wakitarajia upepo wa buruda utawaliwaza vatikan.Lakini Johanna Paulo wa pili alishikilia msimamo wake mkakamavu na baadhi ya wakati ujumbe wake ulionekana kama kishindo-Hakuna aliyeshangaa lakini akizingatia ukweli kwamba ametokea katika kanisa la Poland katika enzi za ukoministi"

Nalo gazeti la OFFENBACH-POST linaandika:

Ile hali kwamba maelfu kwa maelfu ya vijana wamekusanyika kwa amani katika uwanja wa Peter kwaajili ya kipenzi chao,kumsomea na kumuombea Karol WOJTYLA,mnamo masaa ya mwisho mwisho ya maisha yake,nyoyo zao zimekunjuka,inatoa sura ya matumaini mema ya kuendelezwa maadili mema-kama mwenyewe Johanna Paulo wa pili alivyoyapigania.Mtu akitilia maanani maradhi yake ya muda mrefu na jinsi alivyokua katika hali ya kuiaga dunia tangu ijumaa iliyopita,,hatokosa kuamini,na wala hatakosea pia akisema:Mngu yu karibu:

Naalo gazeti la Tageszeitung la mjini Berlin linahisi:

Imani,uadilifu na hali ya kimambo leo,-katika hali ya mchanganyiko kama hiyo mvutanio haukosekanani–mvutano wa ndani kanisani na hata kwengineko ulimwenguni.Lakini daima mtu asisahau; anaetaka kuendeleza anabidi arekebishe.Alikua akifanya vivyo hivyo,japo sio kila wakati kwa kuzingatia wakati tulionao.Johannes Paulo wa Pili amefanikiwa kuutanabahishia ulimwengu,hata maradhi yanastahiki heshma,watu wakubali kinachowafika ,kwa maneno mengine watu wawe na subira.