1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafuriko yauwa 31 Tamil Nadu India

22 Desemba 2023

Watu 31 wamepoteza maisha kufuatia mafuriko na mvua kubwa iliyonyesha katika jimbo la kusini mwa India la Tamil Nadu wiki hii.

https://p.dw.com/p/4aUo9
Indien | Überschwemmung, Monsunregen in Chennai
Picha: Sri Loganathan/ZUMA Press Wire/picture alliance

Mvua kubwa zimeathiri shughuli za kawaida katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo ikiwemo kuharibu barabara na njia ya reli, siku chache baada ya kimbunga kupiga eneo la pwani ya kusini mashariki mwa India na kusababisha uharibifu mkubwa.Waziri wa fedha wa India Nirmala Sithraman amewaambia waandishi wa habari kuwa, idadi ya waliofariki inaweza kuongezeka na kueleza kuwa, zaidi ya watu 40,000 wameokolewa na kwamba juhudi za uokoaji zinaendelea.Idaraya hali ya hewa imesema jimbo la Tamil Nadu limerekodi zaidi ya milimita 64 za mvua wiki hii, kiasi hicho kikiwa mara tatu zaidi ya kawaida. Idara hiyo ya hali ya hewa imetahadharisha kuwa mvua zaidi inatarajiwa kunyesha katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo katika muda wa siku tano zijazo.