1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu ya Wauighur wanafanyishwa kazi kwa lazima

15 Desemba 2020

Wanaharakati wa haki za binaadamu wameikosowa China kwa kuwalazimisha maelfu ya Waislamu wa Wauighur, Xinjiang kufanya kazi ya kuvuna pamba kwa mkono na kuwafunga kwenye kambi za mateso

https://p.dw.com/p/3mjzg
China Baumwoll-Anbau
Picha: Getty Images/AFP

Ripoti ya shirika la Global Policy lililo na makao yake jijini Washington, Marekani, iliyochapishwa Jumatatu inasema mnamo 2018 mikoa mitatu ya Uighur ndani ya jimbo la Xinjiang ilituma watu wasiopungua 570,000 kuvuna pamba kama sehemu ya mpango wa serikali wa kulazimisha uhamishaji wa wafanyakazi.

Watafiti wanakadiria kuwa idadi jumla ya iliyotolewa kuwa inahusika katika kulazimishwa kuvuna pamba kwenye eneo hilo ambalo shughuli zake nyingi za kikazi zinaendeshwa kwa mikono huenda ikawa ya juu zaidi kuliko iliyotolewa.

Xinjiang ni kitovu cha zao la pamba, ikizalisha zaidi ya asilimia 20 ya pamba ulimwenguni. Ripoti ya Global Policy iliyotokana na nyaraka za serikali ya China zinazopatikana mtandaoni inaonya juu ya "athari mbaya" katika usambazaji wa zao hilo ulimwengu.

Ripoti hiyo aidha inadokeza kuwa wafungwa wengi wa zamani wamehamishiwa katika maeneo ya kufanya kazi za kiwango cha chini viwandani wakati China inasema kuwa wafungwa wote "wamehitimu" kutoka vituo hivyo. Soma zaidi Wapi watakwenda wafungwa wa Jela la Guantanamo? 

DW Investigativ Projekt: Uiguren Umerziehungslager in China ACHTUNG SPERRFRIST 17.02.2020/17.00 Uhr MEZ
Picha hii iliyopigwa mnamo Mei 31, 2019 inaonyesha minara kwenye kituo cha usalama karibu na kile kinachodhaniwa kuwa kambi ya mafunzo ambapo makabila mengi ya Waislamu wamefungwa, katika mkoa wa Xinjiang kaskazini magharibi mwa China.Picha: AFP/G. Baker

Uhamisho unaendeshwa kijeshi

Inadaiwa kuwa walio na jukumu la kuendesha mpango wa uhamishaji wa wafanyakazi wanachunguzwa sana na polisi, na uhamisho wa hatua kwa hatua unaendeshwa chini ya usimamizi kwa mtindo wa kijeshi na mafunzo ya kiitikadi.

Kulingana na Adrian Zenz, ambaye aliweka bayana nyaraka hizo za serikali, ni wazi kwamba uhamisho wa wafanyakazi wa kuvuna pamba unajumuisha hatari kubwa sana ya kazi ya kulazimishwa. Soma zaidi Michafuko ya Wa-Uigur katika Mkoa wa Xinjiang, China

Adrian amesema baadhi ya wafanyakazi hao kwa kiwango cha chini wanaonesha kukubali kwa idhini yao kuhusika katika mchakato huo kutokana na kufaidika kifedha, lakini haiwezekani kufafanua ni muda gani inafikia baadhi yao kukubali baada ya kulazimishwa.

Ripoti hiyo pia inasema kuna motisha ya kiitikadi ya kuutekeleza mpango huo, kwani kuongezeka kwa mapato ya vijijini kunaruhusu maafisa kufikia malengo ya kupunguza umaskini yaliyowekwa na serikali.

Symbolbild Konflikt Uiguren - China | Protest in Washington 2009
Waandamanaji wa jamii ya kiislamu wa Uyghur mkoa wa Xinjiang nchini China,Picha: Michael Reynolds/dpapicture-alliance

Serikali imekanusha

Hata hivyo, China imekanusha vikali madai ya kazi ya kulazimishwa inayohusisha ya Waislamu wa jamii ya Uighur huko Xinjiang, na kuishutumu Marekani kutaka kukandamiza kampuni za Xinjiang. China inasema mipango ya mafunzo, miradi ya kazi na elimu bora imesaidia katika kumaliza ukatili katika eneo hilo.

Mapema mwezi huu, Marekani ilipiga marufuku uagizaji wa pamba inayozalishwa Xinjiang kupitia kampuni moja ya kijeshi ya China, ambayo hutoa theluthi moja ya zao linalozalishwa katika mkoa mzima.

Na katika bunge la Senati la Marekani kuna mswada mwingine uliopendekezwa wa kupiga marufuku uagizaji wote wa pamba kutoka Xinjiang ambao kufikia sasa bado haujapitishwa.

Kulingana na ripoti ya iliyotolewa mwezi Machi na Taasisi ya Sera ya Mkakati ya Australia, baadhi ya kampuni za kimataifa ikiwa ni pamoja na Adidas, Gap na Nike zinashtumiwa kwa kuwatumia Waislamu wa jamii ya Uighur katika kazi za lazima katika usambazaji wa nguo.

 

/AFP