1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Maelfu ya watu waandamana mjini Istanbul dhidi ya Israel

1 Januari 2024

Maelfu ya watu wamejitokeza kwenye maandamano mjini Istanbul katika kuonyesha mshikamano na Wapalestina hii leo huku vita vikiendelea katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4am7Q
Polisi wa kukabiliana na ghasia wazuia waandamanji kuingia mjini kabla ya kuhudhuria mkutano wa hadhara wa Mei day
Waandamanaji nchini UturukiPicha: Sertac Kayar/REUTERS

Picha za televisheni na mitandaoni zimeonyesha waandamanaji hao waliokuwa wakipeperusha bendera za Uturuki na Palestina wakivuka daraja la kati la Galata huko Istanbul, huku baadhi wakivalia vitambaa vya kichwa vya rangi ya kijani inayotumiwa pia na tawi la kijeshi la kundi la Hamas.

Shirika la habari la serikali, Anadolu, limeripoti kuwa wanasiasa kadhaa kutoka chama tawala cha AKP pia walishiriki maandamano hayo.

Soma pia:Uhusiano wa Israel na Uturuki waharibika baada ya Gaza

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki alilaani mashambulizi hayo ya Israel, huku akilitaja kundi la Hamas kuwa "harakati za kupigania ukombozi." Israel na washirika wake wanalitambua kundi hilo kuwa la kigaidi.

Mara kwa mara, Erdogan amekuwa akimshambulia kwa ukali Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa vita vyake katika Ukanda wa Gaza na hivi karibuni alimlinganisha na mtawala wa kinazi wa Ujerumani, Adolf Hitler.

Netanyahu alijibu matamshi hayo kwa kusema kuwa Erdogan anafanya "mauaji ya kimbari" dhidi ya Wakurdi, na kuongeza kuwa kiongozi huyo wa Kituruki hayuko katika nafasi ya kumkosoa.