1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu ya wanawake waandamana Kongo kupinga vita

Sylvia Mwehozi
9 Machi 2024

Waandamanaji hao walitumia Siku ya Kimataifa ya Wanawake iliyoadhimishwa jana katika kuomboleza watu waliouawa kwenye mapigano yaliyolikumba eneo hilo kwa miongo kadhaa.

https://p.dw.com/p/4dKaR
DR Kongo Regen Goma
Wanawake wa KongoPicha: Arlette Bashizi/REUTERS

Maelfu ya wanawake waliovalia mavazi meusi waliandamana jana, kushinikiza amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Waandamanaji hao walitumia Siku ya Kimataifa ya Wanawake iliyoadhimishwa jana katika kuomboleza watu waliouawa kwenye mapigano yaliyolikumba eneo hilo kwa miongo kadhaa.

Maandamano hayo yalifanyika katika mji wa Bukavu na kuwashirikisha wanawake kutoka matabaka mbalimbali, wakiwemo wanasiasa na watu waliokimbia makazi yao.

Waandamanaji walibeba mabango yenye ujumbe uliosomeka kuwa wanawake wa Kongo wanakataa vita, ubakaji na uporaji wa rasilimali za nchi. Mwanaharakati wa haki za wanawake Jeannine Kabyahura, aliyeandamana huko Bunia, alisema kuwa wameamua kuvaa nguo nyeusi ili kuonyesha hasira na masikitiko yao.

Maandamano mengine: Mamia ya wanawake waandamana mjini Kinshasa wakitaka vita ikomeshwe

Kabyahura ameongeza kuwa wanawake wengi wameuawa jimboni Ituri ambapo kwa mwaka huu pekee wanawake 68 tayari wamepoteza maisha katika maeneo ya Djugu na Irumu.