1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Maelfu ya raia wa Niger washerehekea mwaka 1 wa mapinduzi

27 Julai 2024

Maelfu ya watu walikusanyika hapo jana katika mji mkuu wa Niger, Niamey ili kusherehekea mwaka mmoja tangu kufanyike mapinduzi ya kijeshi yaliyomwondoa madarakani Mohamed Bazoum.

https://p.dw.com/p/4iotC
Raia wa Niger wakishangilia mjini Niamey
Raia wa Niger wakishangilia mjini NiameyPicha: AFP

Umati wa watu walisherehekea wakiwa wamevalia nguo zenye picha za viongozi wa serikali, huku wakimlaki kiongozi wa sasa wa nchi hiyo Abdourahamane Tiani ambaye pia alihudhuria sherehe hizo lakini hakutoa hotuba yoyote.

Uwanja kulikodhimishwa hafla hiyo ulikuwa chini ya ulinzi mkali, yakiwemo magari ya kivita yaliyozunguka eneo hilo.

Soma pia:Kiongozi wa kijeshi wa Niger asema nchi hiyo inaelekea kupata "uhuru kamili"

Waziri Mkuu wa Niger Ali Mahaman Lamine Zeine amesema katika historia ya nchi hiyo, hakuna tukio lililopata uungwaji mkono mkubwa kama huo. Maadhimisho ya siku ya mapinduzi ya Julai 26 yalitangazwa kuwa likizo ya umma.