1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madaktari waandamana Ujerumani kupigania hali njema kwao

12 Machi 2024

Maelfu ya madaktari katika hospitali za vyuo vikuu vya Ujerumani wameandamana kudai nyongeza ya mapato na mazingira bora ya kazi.

https://p.dw.com/p/4dPSO
Proteste im Gesundheitswesen | Deutschland
Madaktari wanashikilia mabango yenye maneno "Tuko katika wakati wa mwisho", "Huduma bora ya afya ina bei", "Heshima" na "Madaktari wamechoka kwa sababu ya hatari". Picha: Erbil Basay/AA/picture alliance

Monika Heinold, mpatanishi mkuu wa waajiri amesema yapo matumani ya kufanyika mazungumzo zaidi. Madaktari hao wanadai nyongeza ya mishahara ya asilima 12.5 pamoja na marupurupu ya juu kwa kazi za kawaida za nyakati za usiku, mwishoni mwa juma na likizo za umma.

Kwa mujibu wa chama cha madaktari, Marburger Bund, takriban madaktari 7,000 kutoka hospitali 23 za vyuo vikuu walishiriki maandamano hayo. Awamu ya nne ya mazungumzo kati ya chama cha madaktari na waajiri ambao ni majimbo ya shirikisho ya Ujerumani hayakuwa na matokeo chanya.