1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Maelfu wafukuzwa kazi kwa kushiriki mgomo Iran

29 Aprili 2023

Wafanyakazi elfu nne wa sekta ya mafuta ya petroli wa Iran waliogoma kuhusu malipo na mazingira magumu katika eneo linalozalisha nishati kusini mwa nchi hiyo watafutwa kazi na nafasi zao kujazwa na watu wengine.

https://p.dw.com/p/4QiNf
Rentner Demo in Khuzestan
Picha: AzadEttehad

Afisa mmoja anayesimamia sekta ya mafuta na gesi ya jamhuri ya Kiislamu jana Ijumaa alinukuliwa na shirika la habari la serikali ya Iran-IRNA akisema wafanyikazi hao katika jimbo la  Bushehr wamedai nyongeza ya mishahara na kuboreshwa kwa hali ya malazi na usafiri.Kwa mwaka uliopita wa 2022, Iran ilishuhudia wimbi la migomo ya walimu na madereva wa mabasi ambao walipinga mishahara duni na gharama kubwa za maisha. Tangu mwaka 2018, uchumi wa Iran umekuwa katika athari iliyotokana na vikwazo vya  Marekani na kuongezeka zaidi kutokana na  mfumuko wa bei, pamoja na kuporomoka kwa sarafu yake, rial dhidi ya dola, ikiwa ni baada ya serikali ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya kihistoria ya nyuklia ya Tehran.